Tuesday, November 22, 2022

Maisha ya Chuoni

                  Picha kwa hisani ya Dago Muller

Maisha ya chuo kikuu yanasemekana kuwa ya kufurahiwa na ya kukumbukwa katika maisha ya kila mwanafunzi. Ni wazo lililokwama kichwani mwangu baada ya kupokea barua ya wito iliyokuwa nikiisubiri kwa muda mrefu ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mombasa, kusomea taaluma ya Habari na Mawasiliano ya Umma. Kama ilivyo ndoto ya kila mwanagenzi wa pwani ya kujiunga na chuo cha Mombasa nilijawa na furaha na bashasha kupata fursa hio.Hii ilikuwa Juni 2020, mwaka ambao ulikuwa wenye changamoto ya kipekee ya tishio la kimataifa la Uviko 19. Kwa agizo la serikali la kufungwa kwa taasisi zote za elimu kutokana na ongezeko la virusi vya korona haikuwezekana kujiunga na chuo kikuu kwa wakati huo, na ililazimika kungoja hadi Januari 2021.


Hakika nilifurahi sana kujiunga na chuo kwa sababu ilikuwa inasemekana kwamba kuna Uhuru mwingi sana kama vile kuishi mwenyewe bila ya uangalizi wa mzazi au.mwalimu,sikuweza kungoja kupata Uzoefu huo lakini Hakuna aliyeweza kunionya kuhusu changamoto zake.


Kwa hisani ya Rajaab

Kwa ugumu wa maisha ya chuo ni aghalabu kumpata mwanafunzi wa chuo  kikuu kukaa bila ya kibarua cha ziada ambacho kinaweza kumuingizia kipato cha kujikimu.Ikiwa umefaulu kumaliza chuo bila ya kufanya kibarua basi wewe ni mmoja ya walio bahatika kupata  Ada ya shule kwa muda sahihi.Kwangu haikuwa rahisi ilinilazimu kutafuta vibarua vya hapa na pale ilikuweza kujikimu kimaisha. kwa ugumu huo wa maisha umenifanya kukomaa na kuweza kujielewa zaidi ambapo kwa sasa naeza kukabiliana na changamoto zijazo.

                     Picha kwa Hisani ya Rajaab

Kwangu Chuo ni zaidi ya taasisi ya kujifunzia kwa kuwa imenifundisha mengi mbali na darasani nimekutana na watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii wenye tamaduni, mitazamo, maono, dini na tabia tofauti na imenifanya kujua jinsi ya kuingiliana nao. Kuwa darasani kumekuwa uzoefu mzuri wa kujifunza mambo mapya unapofurahia muda na wengine. Maisha ya kampasi yamenifundisha kubadilishana mawazo na wengi, kufanya kazi kwa ufanisi katika vikundi, kufikia malengo yangu hata katikati ya matatizo.Nilijitahidi sana kuunga urafiki na mtu yeyote ilimradi ni mwanafunzi mwenzangu lakini yote kwa yote nilipata kuelewa mambo mengi na nilijifunza kwamba wanafunzi wengi au watu wengi wanaweza kuwa wakitabasamu na kufurahia lakini ndani kabisa wanakabiliwa na madhila mengi maishani.







Monday, November 7, 2022

VIJANA KAMA CHACHU YA MAENDELEO NCHINI

 

                     Picha Kwa Hisani ya Google

Kenya ina idadi kubwa ya vijana ambao wanasimama kwenye njia ya kuinua uchumi ikiwa watapata fomula sahihi ya kutumia.Hata hivyo vipaji vingi vya vijana vinaoza majumbani kwa sababu hawafanyi lolote la kujenga labda kutokana na kukosa mwongozo sahihi lakini kuna nafasi ya kuboreshwa.Vijana ndio nguzo ya kiuchumi ambayo inaweza kuendesha na kuunda mahitaji ya bidhaa na huduma hasa kutokana na kukua kwa uchumi wa kidijitali. Hata hivyo, pamoja na faida hii kubwa,nchi  pia inakabiliwa na hatari kubwa ya kuhakikisha kuwa vijana wao hawaingii kwenye ghilba za wizi na ujangili ambazo zinaweza kuwafanya kuwa hatari kwenye Jamii.Je, ni kwa jinsi gani Kenya inaweza kujiweka katika nafasi ya kufaidika na idadi ya watu wachanga?


                     Picha Kwa Hiasani ya Google

Wakati nchi inatazamia kufikia malengo yake ya maendeleo,miongoni mwa maono ya 2030 na Malengo ya maendeleo endelevu(SDG),inapaswa kuweka wazi majukumu ya vijana katika kuyafikia na kuwashirikisha kisiasa,kijamii na hata kiuchumi.Ikiwa Kenya itabeba kipengele kimoja tu muhimu zaidi cha kuwawezesha vijana kwa kuwapa ujuzi unaohitajika wa kifedha,itakuwa na uhakika wa kuua ndege wawili kwa jiwe moja kwa kuwa haitakuza tu tija yake kama ya nchi bali pia kuwasaidia kujenga ufumbuzi wa kudumu wa kiuchumi kwa wao na familia zao.


                        Picha Kwa Hisani ya Google

Aidha,vijana nchini wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mafanikio hayo ya kiuchumi kwa kujitosa katika sekta kama vile shughuli za kibiashara,kilimo na kuchuma kutokana na vipaji vyao,Sehemu za ujasiriamali zitahimiza uvumbuzi wa teknolojia mpya ili kupata tija.Ufanisi wa biashara hizi na kiwango cha juu cha ushuru unaotozwa unachochea ukuaji wa nchi.Uwepo wa mfumo wa kidijitali ni jukwaa jingine la vijana kujihusisha na kazi za mitandaoni,kuanzisha biashara ndogo ndogo,kutoa huduma za ushauri na mengine kwenye orodha hii.



                    Picha Kwa Hisani ya Google

Mashirika ya kiserikali na kibinafsi yanapaswa pia kutoa mafunzo ya uwongozi kwa vijana na ujuzi wa kifikiri kwa kina kwani hii itakuwa muhimu katika kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao yote,kwa nini iwe hivi? Kwa sababu kijana bora hahakikishii tu mafanikio ya kizazi kilichopo bali kwa hata vizazi vijavyo.


                                                        By   Dago Rajab

Monday, October 24, 2022

MABADILIKO YA TABIA NCHI

            [Picha kwa Ihsani ya Pinterest]

Nini maana halisi ya Mabadiliko ya tabia nchi? Ni madiliko yanayo sababishwa na kubadilika kwa hali ya hewa inayokaa kwa mda mrefu ambayo inaleta athari duniani.Watu wingi hudhani Ukame pekee ndio huletwa na mabadiliko ya tabia nchi ila sivyo,hali yeyote ya hewa inapokaa kwa mda mrefu na kuleta athari kubwa hayo ni mabadiliko ya tabia nchi.Hatuwezi kuzungumzia mabadiliko ya tabia nchi bila kuzungumzia kiwango cha joto kinachozidi kila uchao kwa sababu kuongezeka au kupungua kwa joto ndio huleta mabadiliko ya tabia nchi Ulimwenguni.                                                                                

                    
[Picha kwa Ihsani ya Google.]

Tangu mwaka 1950 mapinduzi ya viwanda yalipotokea Joto katika uso wa dunia limeongezeka kwa nyuzi joto 0.8 na hiyo imesababishwa hasa na shughuli za kibinadamu ambazo zimeongeza kiwango cha gesi joto[global warming]katika anga,kuongezeka huko kumepelekea tabaka la Ozoni lenye kazi ya kudhibiti kiwango cha joto kinacho ingia na kutoka kwenye Uso wa dunia kuharibika na kushindwa kudhibiti kiwango cha joto kinacho ingia na kutoka.Ongezeko hilo linaweza kuonekana dogo Sana kwa akili ya kawaida ya binadamu lakini lina athari kubwa sana kwenye uso wa dunia.


Kumekuwa na harakati mbalimbali zinazo fanyika ili kupunguza kiwango cha joto ulimwenguni zikiwemo Harakati za kutoa elimu kwa Raia kuhusu athari za mabadiliko ya hali ya hewa na jinsi ya kukabiliana na janga hilo.Pili, kuna harakati za nchi kupunguza uzalishaji wa gesi joto kwenye viwanda vyao ambavyo ndio chanzo namba moja cha uharibifu wa hali ya hewa.Pia kumekuwa na jitihada mbalimbali za wananchi  kulazimisha serikali zao kuchukua hatua muafaka za kukabiliana na janga hili kupitia midahalo na maandamano.


Wakati wanasayansi wanasema  kuongeza kwa Nyuzi joto 2 kutaiweka dunia katika hali ya hatari,ripoti ya mwaka 2013 ya IPCC inaonyesha kuwa kiwango cha joto kitaongezeka hadi nyuzi 1.5 kufikia mwishoni mwa karne ya 21 kama hakuta chukuliwa hatua  zozote,Aidha ripoti hio imesema mabadiliko ya tabia nchi yanaweza kukabiliwa endapo tu dunia kwa ujumla itafanya mabadiliko kwenye maeneo mengi.


                  [Picha kwa Ihsani ya Google]

Athari ambazo zitaendela kuikumba dunia endapo hatutachukua hatua mwafaka ni kupanda kwa Kiwango cha maji baharini ambapo itapelekea baadhi ya Visiwa kufurika na vengine kuzama kabisa.Shirika la  Afya Duniani "WHO" limeonya kuwa mabadiliko hayo yatapelekea kuongezeka kwa magonjwa kama Nimonia na Utapiamlo ambao unasababishwa na ukosefu wa lishe bora ambao utakuwa ni tatizo kubwa kwa nchi za Afrika.Makadirio ya WHO yanaonyesha watu 140,000 hupoteza maisha kila mwaka kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.

Ni jukumu letu sote  kukabiliana na janga hili na kuhakisha lina tokomea.

                                                             By Dago Rajaab.


Monday, October 17, 2022

FAHARI YA PWANI

                 Picha Kwa Hisani ya Google

Tangu jadi halmashauri ya Bandari ya Mombasa imekuwa Fahari ya wakaazi wa mvita na pwani kwa ujumla kwa sababu imekuwa ikitoa fursa nyingi zikiwemo kuajiri maelfu ya wakaazi wa pwani na imekuwa ikitoa Fursa ya kuendesha shughuli za Uchukuzi zikiwemo biashara ya Usafirishaji wamizigo ambazo pia kivyake zimeajiri mamia ya watu ambao wanategemea bandari ili kuendesha maisha yao ya kila Uchao.

                 Picha Kwa Hisani ya Google

Mnamo Disemba mwaka 2019 fahari hii iliingia doa pindi tu Rais Mstaafu Uhuru kenyatta alipo agiza shughuli za Halmashauri ya bandari ya Mombasa kuhamishwa kwenye kaunti ndogo ya Naivasha,Habari hii ili watamausha wa Pwani na wapo wachache walio simama kidete kupinga udhalili huo,akiwemo aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Mvita Mheshimiwa Abduswamad ambapo hakufanikiwa kuupinga uamuzi huo.

Kitendo hiki kilipelekea maelfu ya  watu kupoteza ajira na kuzidi kuzorotesha uchumi wa wananchi wa pwani ambao walizalimika kuukumbatia Umaskini na Umaskini ukawa vazi Lao.

Ni miezi kadhaa sasa imepita tangu tumeingia debeni na kupiga kura kilio chetu kikubwa kilikuwa kurudishwa kwa shughuli zote za Halmashauri ya bandari ndani ya Pwani iliziweze kuwafaidisha wazawa,Rais William Ruto aliinuka kidedea na kuamrisha mara moja shughuli zote kurejeshwa rasmi kwenye bandari ya mombasa.

Wakaazi walipongeza kwa hatua hii kwa sababu Ukiritimba wa S.G.R juu ya uchukuzi wa Mizigo umeharibu uchumi wa bandari ya Mombasa katika kipindi cha miaka mitatu ambapo maelfu ya wamiliki wa lori na madereva walipoteza maisha yao ambapo vituo vya kigeni vya kontena vilikosa manufaa na maelfu ya watu wanaofanya kazi katika uuzaji wa malori, vituo vya huduma ya mafuta, mitambo, wafanyabiashara wa vipuri waliachwa bila kazi.


                  Picha Kwa Hisani ya Google

Kongole kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais William Ruto kwa kuondosha udhalimu huu na tuendelee kumuombea kwa Maulana azidi kuendelea kutatua madhila ya pwani.

                                                       By Dago Rajaab.

Monday, October 10, 2022

Tragic Campus realationship,When to call it Quit.


                         Picture Courtesy of Google 

Tragic Campus Relationships, When to Call it Quit.


Romantic relationships in colleges and universities are fast growing. It is common now to see campus couples having moments of public display of affection. A recent study shows that up to 70% of students in Kenyan universities have at some point been in a relationship. While these unions look rosy to the public, the real trouble is hiding out. Campus relationships have more often than not turned tragic. How do you know when time's up in a toxic relationship?


When you feel emotionally abused,  you might consider taking time off and focusing on your self growth. Emotional abuse comes in form of acts of dominance, belittlement and outright ignorance. When you feel this, do not wait for the worst to happen.


Second is distance. If you feel your partner growing distant, it might be time to call it quits. Distance is a show of disinterest and emotional detachment. It could mean that your partner has shifted emotionally and any reaction could spark an argument.


Verbal abuse is a common sign before relationships turn tragic. Most couples that report physical abuse had first been abused verbally in the relationship. Do not ignore it when your partner is saying words that hurt or demean you.


Lastly, physical abuse is the last thing you want to be a victim of. If you have once been in a situation of being physically abused, you know better than risk a second incident.


Do not wait until it is too late. You know what to look out for. When you spot any of these, your relationship is probably slipping away and turning violent.


                                                      By Dago Rajaab

Sunday, October 2, 2022

MFAHAMU MAGAWA


Picha kwa Hisani ya Google 

Mfahamu magawa panya ambaye ametunukiwa nishani ya dhahabu kwa ushujaa wake wakuweza kunusa vilipuzi kwa kiwango cha juu sana.


Katika maisha yake ya miaka nane panya huyu aliweza kunusa mabomu 100 ya ardhini na vilipuzi vingine vingi ambavyo havikulipuka nchini Cambodia.

Cambodia ilikuwa moja ya nchi ambayo imeshiriki kikamilifu katika vita vya dunia kwa hivyo moja ya athari kumbwa ambayo ipo hadi sasa ni vilipuzi vingi ambavyo vipo ardhini ambavyo vilifukiwa na havija tenguliwa.

Kulikuwa na haja ya kutafuta mbinu m'badala ya kutengua mabomu hayo bila ya kuhatarisha uhai wa Binadamu.Hapo ndipo shirika la Apopo ambalo limesajiliwa nchini Ubelgiji lilikuja na wazo la kumfunza panya ambaye anauwezo mkumbwa wa kunusa ilikuwasaidia kutengua vilipuzi hivyo.

Magawa akiwa amefunzwa kugundua kemikali ndani ya vilipuzi aliweza kusafisha zaidi ya mita za mraba 141,000,Sawa na viwanja ishirini vya mpira wa miguu.

Panya huyo alikuwa na uwezo wa kupekuwa uwanja wa ukumbwa wa kiwanja cha  tenisi kwa muda wa Dakika 20 tu jambo ambalo lingewachukuwa binadamu wenye detector ya chuma siku tatu hadi nne.

Mnamo mwaka 2020 Magawa alitunikiwa medali ya dhahabu ya PDSA ambayo ni heshima ya juu zaidi kwa wanyama kwa kujitolea kwake kuokoa maisha ya watu wengi.Pia  alikuwa panya wa kwanza kutunukiwa medali hiyo katika historia ya miaka 77 ya Shirika hilo.

Magawa alistaafu juni,2020 baada ya kupunguza kasi ya utendaji kazi kwa sababu ya uzee na baadaye kufariki mnamo tarehe 11 January mwaka 2022 ambapo alikuwa amefikisha umri wa miaka nane nikimnukuu mmoja wa wauguzi ambao walikuwa wakimuhudumia alisekuwa panya huyo alifariki kwa amani akiwa chini ya uangalizi wa madaktari.

                                                      By Dago Rajaab
            

Maisha ya Chuoni

                  Picha kwa hisani ya Dago Muller Maisha ya chuo kikuu yanasemekana kuwa ya kufurahiwa na ya kukumbukwa katika maisha ya kil...