Tuesday, November 22, 2022

Maisha ya Chuoni

                  Picha kwa hisani ya Dago Muller

Maisha ya chuo kikuu yanasemekana kuwa ya kufurahiwa na ya kukumbukwa katika maisha ya kila mwanafunzi. Ni wazo lililokwama kichwani mwangu baada ya kupokea barua ya wito iliyokuwa nikiisubiri kwa muda mrefu ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mombasa, kusomea taaluma ya Habari na Mawasiliano ya Umma. Kama ilivyo ndoto ya kila mwanagenzi wa pwani ya kujiunga na chuo cha Mombasa nilijawa na furaha na bashasha kupata fursa hio.Hii ilikuwa Juni 2020, mwaka ambao ulikuwa wenye changamoto ya kipekee ya tishio la kimataifa la Uviko 19. Kwa agizo la serikali la kufungwa kwa taasisi zote za elimu kutokana na ongezeko la virusi vya korona haikuwezekana kujiunga na chuo kikuu kwa wakati huo, na ililazimika kungoja hadi Januari 2021.


Hakika nilifurahi sana kujiunga na chuo kwa sababu ilikuwa inasemekana kwamba kuna Uhuru mwingi sana kama vile kuishi mwenyewe bila ya uangalizi wa mzazi au.mwalimu,sikuweza kungoja kupata Uzoefu huo lakini Hakuna aliyeweza kunionya kuhusu changamoto zake.


Kwa hisani ya Rajaab

Kwa ugumu wa maisha ya chuo ni aghalabu kumpata mwanafunzi wa chuo  kikuu kukaa bila ya kibarua cha ziada ambacho kinaweza kumuingizia kipato cha kujikimu.Ikiwa umefaulu kumaliza chuo bila ya kufanya kibarua basi wewe ni mmoja ya walio bahatika kupata  Ada ya shule kwa muda sahihi.Kwangu haikuwa rahisi ilinilazimu kutafuta vibarua vya hapa na pale ilikuweza kujikimu kimaisha. kwa ugumu huo wa maisha umenifanya kukomaa na kuweza kujielewa zaidi ambapo kwa sasa naeza kukabiliana na changamoto zijazo.

                     Picha kwa Hisani ya Rajaab

Kwangu Chuo ni zaidi ya taasisi ya kujifunzia kwa kuwa imenifundisha mengi mbali na darasani nimekutana na watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii wenye tamaduni, mitazamo, maono, dini na tabia tofauti na imenifanya kujua jinsi ya kuingiliana nao. Kuwa darasani kumekuwa uzoefu mzuri wa kujifunza mambo mapya unapofurahia muda na wengine. Maisha ya kampasi yamenifundisha kubadilishana mawazo na wengi, kufanya kazi kwa ufanisi katika vikundi, kufikia malengo yangu hata katikati ya matatizo.Nilijitahidi sana kuunga urafiki na mtu yeyote ilimradi ni mwanafunzi mwenzangu lakini yote kwa yote nilipata kuelewa mambo mengi na nilijifunza kwamba wanafunzi wengi au watu wengi wanaweza kuwa wakitabasamu na kufurahia lakini ndani kabisa wanakabiliwa na madhila mengi maishani.







Monday, November 7, 2022

VIJANA KAMA CHACHU YA MAENDELEO NCHINI

 

                     Picha Kwa Hisani ya Google

Kenya ina idadi kubwa ya vijana ambao wanasimama kwenye njia ya kuinua uchumi ikiwa watapata fomula sahihi ya kutumia.Hata hivyo vipaji vingi vya vijana vinaoza majumbani kwa sababu hawafanyi lolote la kujenga labda kutokana na kukosa mwongozo sahihi lakini kuna nafasi ya kuboreshwa.Vijana ndio nguzo ya kiuchumi ambayo inaweza kuendesha na kuunda mahitaji ya bidhaa na huduma hasa kutokana na kukua kwa uchumi wa kidijitali. Hata hivyo, pamoja na faida hii kubwa,nchi  pia inakabiliwa na hatari kubwa ya kuhakikisha kuwa vijana wao hawaingii kwenye ghilba za wizi na ujangili ambazo zinaweza kuwafanya kuwa hatari kwenye Jamii.Je, ni kwa jinsi gani Kenya inaweza kujiweka katika nafasi ya kufaidika na idadi ya watu wachanga?


                     Picha Kwa Hiasani ya Google

Wakati nchi inatazamia kufikia malengo yake ya maendeleo,miongoni mwa maono ya 2030 na Malengo ya maendeleo endelevu(SDG),inapaswa kuweka wazi majukumu ya vijana katika kuyafikia na kuwashirikisha kisiasa,kijamii na hata kiuchumi.Ikiwa Kenya itabeba kipengele kimoja tu muhimu zaidi cha kuwawezesha vijana kwa kuwapa ujuzi unaohitajika wa kifedha,itakuwa na uhakika wa kuua ndege wawili kwa jiwe moja kwa kuwa haitakuza tu tija yake kama ya nchi bali pia kuwasaidia kujenga ufumbuzi wa kudumu wa kiuchumi kwa wao na familia zao.


                        Picha Kwa Hisani ya Google

Aidha,vijana nchini wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mafanikio hayo ya kiuchumi kwa kujitosa katika sekta kama vile shughuli za kibiashara,kilimo na kuchuma kutokana na vipaji vyao,Sehemu za ujasiriamali zitahimiza uvumbuzi wa teknolojia mpya ili kupata tija.Ufanisi wa biashara hizi na kiwango cha juu cha ushuru unaotozwa unachochea ukuaji wa nchi.Uwepo wa mfumo wa kidijitali ni jukwaa jingine la vijana kujihusisha na kazi za mitandaoni,kuanzisha biashara ndogo ndogo,kutoa huduma za ushauri na mengine kwenye orodha hii.



                    Picha Kwa Hisani ya Google

Mashirika ya kiserikali na kibinafsi yanapaswa pia kutoa mafunzo ya uwongozi kwa vijana na ujuzi wa kifikiri kwa kina kwani hii itakuwa muhimu katika kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao yote,kwa nini iwe hivi? Kwa sababu kijana bora hahakikishii tu mafanikio ya kizazi kilichopo bali kwa hata vizazi vijavyo.


                                                        By   Dago Rajab

Maisha ya Chuoni

                  Picha kwa hisani ya Dago Muller Maisha ya chuo kikuu yanasemekana kuwa ya kufurahiwa na ya kukumbukwa katika maisha ya kil...