Picha kwa hisani ya Dago Muller
Maisha ya chuo kikuu yanasemekana kuwa ya kufurahiwa na ya kukumbukwa katika maisha ya kila mwanafunzi. Ni wazo lililokwama kichwani mwangu baada ya kupokea barua ya wito iliyokuwa nikiisubiri kwa muda mrefu ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Ufundi cha Mombasa, kusomea taaluma ya Habari na Mawasiliano ya Umma. Kama ilivyo ndoto ya kila mwanagenzi wa pwani ya kujiunga na chuo cha Mombasa nilijawa na furaha na bashasha kupata fursa hio.Hii ilikuwa Juni 2020, mwaka ambao ulikuwa wenye changamoto ya kipekee ya tishio la kimataifa la Uviko 19. Kwa agizo la serikali la kufungwa kwa taasisi zote za elimu kutokana na ongezeko la virusi vya korona haikuwezekana kujiunga na chuo kikuu kwa wakati huo, na ililazimika kungoja hadi Januari 2021.
Hakika nilifurahi sana kujiunga na chuo kwa sababu ilikuwa inasemekana kwamba kuna Uhuru mwingi sana kama vile kuishi mwenyewe bila ya uangalizi wa mzazi au.mwalimu,sikuweza kungoja kupata Uzoefu huo lakini Hakuna aliyeweza kunionya kuhusu changamoto zake.
Kwa ugumu wa maisha ya chuo ni aghalabu kumpata mwanafunzi wa chuo kikuu kukaa bila ya kibarua cha ziada ambacho kinaweza kumuingizia kipato cha kujikimu.Ikiwa umefaulu kumaliza chuo bila ya kufanya kibarua basi wewe ni mmoja ya walio bahatika kupata Ada ya shule kwa muda sahihi.Kwangu haikuwa rahisi ilinilazimu kutafuta vibarua vya hapa na pale ilikuweza kujikimu kimaisha. kwa ugumu huo wa maisha umenifanya kukomaa na kuweza kujielewa zaidi ambapo kwa sasa naeza kukabiliana na changamoto zijazo.
Picha kwa Hisani ya Rajaab
Kwangu Chuo ni zaidi ya taasisi ya kujifunzia kwa kuwa imenifundisha mengi mbali na darasani nimekutana na watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi hii wenye tamaduni, mitazamo, maono, dini na tabia tofauti na imenifanya kujua jinsi ya kuingiliana nao. Kuwa darasani kumekuwa uzoefu mzuri wa kujifunza mambo mapya unapofurahia muda na wengine. Maisha ya kampasi yamenifundisha kubadilishana mawazo na wengi, kufanya kazi kwa ufanisi katika vikundi, kufikia malengo yangu hata katikati ya matatizo.Nilijitahidi sana kuunga urafiki na mtu yeyote ilimradi ni mwanafunzi mwenzangu lakini yote kwa yote nilipata kuelewa mambo mengi na nilijifunza kwamba wanafunzi wengi au watu wengi wanaweza kuwa wakitabasamu na kufurahia lakini ndani kabisa wanakabiliwa na madhila mengi maishani.



Nakala Safi 👏👏
ReplyDeleteHeko
ReplyDeleteKuntu kabisa
ReplyDeleteNakala nzuri.Heko
ReplyDeleteGood one
ReplyDeleteBest 👍🏽
ReplyDeleteKazi safiiiii kaka
ReplyDeleteNakala yako ina ubunifu tena nakubaliana nawe kwamba Ikiwa umefaulu kumaliza chuo bila ya kufanya kibarua basi wewe ni mmoja ya walio bahatika
ReplyDeleteHongera
ReplyDeleteKuntu kaka👏👏👏
ReplyDeleteSwadakta kabisa
ReplyDeleteKazi safi