Picha Kwa Hisani ya Google
Kenya ina idadi kubwa ya vijana ambao wanasimama kwenye njia ya kuinua uchumi ikiwa watapata fomula sahihi ya kutumia.Hata hivyo vipaji vingi vya vijana vinaoza majumbani kwa sababu hawafanyi lolote la kujenga labda kutokana na kukosa mwongozo sahihi lakini kuna nafasi ya kuboreshwa.Vijana ndio nguzo ya kiuchumi ambayo inaweza kuendesha na kuunda mahitaji ya bidhaa na huduma hasa kutokana na kukua kwa uchumi wa kidijitali. Hata hivyo, pamoja na faida hii kubwa,nchi pia inakabiliwa na hatari kubwa ya kuhakikisha kuwa vijana wao hawaingii kwenye ghilba za wizi na ujangili ambazo zinaweza kuwafanya kuwa hatari kwenye Jamii.Je, ni kwa jinsi gani Kenya inaweza kujiweka katika nafasi ya kufaidika na idadi ya watu wachanga?
Picha Kwa Hiasani ya Google
Wakati nchi inatazamia kufikia malengo yake ya maendeleo,miongoni mwa maono ya 2030 na Malengo ya maendeleo endelevu(SDG),inapaswa kuweka wazi majukumu ya vijana katika kuyafikia na kuwashirikisha kisiasa,kijamii na hata kiuchumi.Ikiwa Kenya itabeba kipengele kimoja tu muhimu zaidi cha kuwawezesha vijana kwa kuwapa ujuzi unaohitajika wa kifedha,itakuwa na uhakika wa kuua ndege wawili kwa jiwe moja kwa kuwa haitakuza tu tija yake kama ya nchi bali pia kuwasaidia kujenga ufumbuzi wa kudumu wa kiuchumi kwa wao na familia zao.
Picha Kwa Hisani ya Google
Aidha,vijana nchini wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mafanikio hayo ya kiuchumi kwa kujitosa katika sekta kama vile shughuli za kibiashara,kilimo na kuchuma kutokana na vipaji vyao,Sehemu za ujasiriamali zitahimiza uvumbuzi wa teknolojia mpya ili kupata tija.Ufanisi wa biashara hizi na kiwango cha juu cha ushuru unaotozwa unachochea ukuaji wa nchi.Uwepo wa mfumo wa kidijitali ni jukwaa jingine la vijana kujihusisha na kazi za mitandaoni,kuanzisha biashara ndogo ndogo,kutoa huduma za ushauri na mengine kwenye orodha hii.
Picha Kwa Hisani ya Google
Mashirika ya kiserikali na kibinafsi yanapaswa pia kutoa mafunzo ya uwongozi kwa vijana na ujuzi wa kifikiri kwa kina kwani hii itakuwa muhimu katika kufanya maamuzi sahihi katika maisha yao yote,kwa nini iwe hivi? Kwa sababu kijana bora hahakikishii tu mafanikio ya kizazi kilichopo bali kwa hata vizazi vijavyo.
By Dago Rajab




Swadakta
ReplyDeleteGood work 👏
ReplyDeleteKazi safi
ReplyDeleteKaz saf
ReplyDeleteKazi safi kaka
ReplyDeleteInafunza Mambo mengi
Kazi nzuri
ReplyDeleteCould not have been said any better..kazi mufti
ReplyDeleteKazi kwa vijana
ReplyDeleteGreat 👌
ReplyDeleteKazi nzuriii
ReplyDeleteGood work
ReplyDeleteNakala nzuri.
ReplyDeleteNakala Safi
ReplyDelete